Wanasheria wizara ya mambo ya ndani ya nchi wanolewa uchambuzi wa mikataba
Ni mafunzo ya siku tatu yaliyoandaliwa na Wizara na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yenye lengo la kuwajengea uwezo Wanasheria kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na Vyombo vya Usalama kufanya uchambuzi wa mikataba na kuepuka kuiingiza Serikali katika hasara, mafunzo yaliyofunguliwa Machi 13, 2024 na Katibu Mkuu wa Wizara Kaspar Mmuya katika Chuo cha Kikanda TRITA Moshi.








