Watu 40 wameuwawa na wengine 100 kujeruhiwa Nchini Urusi, kundi la ISS wamesema wanahusika
Watu 40 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa Nchini Urusi usiku huu baada ya Watu wenye silaha ambao wameficha sura zao (kininja) kuwashambulia kwa risasi Watu ambao walikuwa kwenye Tamasha katika eneo la Crocus City Hall ambalo hutumika kwa shughuli za muziki na kuna maduka yanayouza bidhaa mbalimbali karibu na Mji Mkuu, Moscow ambapo wamelipua eneo hilo na kusababisha moto mkubwa.
Vyombo vya Habari vya Urusi vimeripoti kuwa shambulizi hilo ambalo linatajwa kuwa la kigaidi ni miongoni mwa mashambulizi mabaya kuwahi kutokea Nchini Urusi katika siku za karibuni
Siku mbili kama ya tukio wana usalama wa Marekani walimtaarifu Raisi Putin kuwa kuna wasiwasi washambulio nchini kwakwe kutoka kwa wanamgambo wa Iss ila Riasi Putin alipuuziaa taarifa hiyo
The video credits to @Skynews









