Sasa ni zamu za mtambo wa mabao, Simu ziite tukutane kwa Mkapa

𝐒𝐀𝐒𝐀 𝐍𝐈 π™π€πŒπ” π˜π€ πŒπ“π€πŒππŽ 𝐖𝐀 πŒπ€ππ€πŽ

β€œUongozi na benchi la ufundi wameazimia kwa pamoja kuwa mchezo wetu dhidi ya Mamelodi Sundowns, akabidhiwe kijana kutoka Kizimkazi, Mudathir Yahya. Slogani yetu kwenye mechi hii ‘SIMU ZIITE TUKUTANE KWA MKAPA’ Kazi ambayo tunayo kuanzia sasa hivi ni kupiga simu kwa watu wote tuwaambie tukutane kwa Mkapa”

π’πˆπŒπ” π™πˆπˆπ“π„ π“π”πŠπ”π“π€ππ„ πŠπ–π€ πŒπŠπ€ππ€

β€œWiki hii kazi ni moja tu, tunampigia kila Mtanzania kuwaeleza kuwa jambo ni moja tu kukutana kwa Mkapa, waambieni hata hao Mamelodi Sundowns, agenda ya wiki hii ni simu ziite kama upo ofisini kuna simu ya ofisi itumie piga kwa mtu yoyote unayemjua mwambie unahitajika kwa Mkapa, mpigie shabiki wa timu yoyote mwambie aje Mkapa afurahi”

π“π€π€π‘πˆπ…π€ 𝐙𝐀 π€π…π˜π€ π˜π€ π–π€π‚π‡π„π™π€π‰πˆ 𝐖𝐄𝐓𝐔

β€œZawadi Mauya yupo tayari kufanya kazi kubwa dhidi ya Mamelodi Sundowns, Kibwana Shomari anaendelea vizuri, Yao bado ni 50/50 alichanika nyama za paja, Pacome alikuwepo kwenye kikosi cha Ivory Coast dhidi ya Benin na yupo fit kwa zaidi ya 80% na Aucho anaendelea kujifua kujipanga dhidi ya Mamelodi Sundown

πŒπ“π€πŒππŽ 𝐖𝐀 πŒπ€ππ€πŽ πŒπ”πƒπ€, πŒπ™πˆπ™π„ 𝐍𝐀 𝐁𝐀𝐂𝐂𝐀 𝐖𝐀𝐑𝐄𝐉𝐄𝐀 π€π•πˆπ‚

β€œTunashukuru Shirikisho la Soka Tanzania kwa kuwaruhusu wachezaji wetu ambao walikuwa kambi ya timu ya Taifa kurejea kambini mapema kwa ajili ya maandalizi dhidi ya Mamelodi, nyota hao tayari wamejiunga na jeshi la AVIC tayari kwa maandalizi madhubuti”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button