Wawili Mbaroni Kwa Tuhuma Za KuumwaNdugu Yao na Kumzika Kwenye Shimo la Maji Taka
Wawili Mbaroni Kwa Tuhuma Za Kuumwa Ndugu Yao na Kumzika Kwenye Shimo la Taka
Wawili mbaroni kwa tuhuma za kumuua ndugu yao na kumzika kwenye shimo la maji machafu Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limewakamata na kuwashikilia watuhumiwa wawili Fred Rajabu Chaula na Bashir Richard Chaula kwa tuhuma za
kula njama na kumuua Regina Chaula miaka 62 mkazi wa Bahari Beach Kinondoni Dar es salaam na Denmark.
Akizungumza na waandishi wa habari jjini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro
Jumanne Muliro amesema mwanamke huyo
ambaye alikuwa na kesi zake za madai Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi dhidi ya watuhumiwa na watu wengine alipotea ghafla na hakuonekana tangu Desemba 13,
mwaka jana.
Amesema Jeshi Hilo lilifanya jitihada kubwa za kufuatilia na kuendelea kutilia mashaka maeneo na watu mbalimbali ambapo
Januari 18, 2025 makachero wa Polisi walilazimika kubomoa shimo la maji machafu liliokuwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na kuukuta mwili wa marehemu Regina Rajabu ukiwa umetupwa na kufichwa kwenye shimo hilo.
“Uchunguzi wa kisayansi unaendelea juu ya tukio hili baya na Jeshi la Polisi linalaani vikali vitendo hivi na litahakikisha kila aliyeshiriki katika mauaji haya ya kinyama anakamatwa na hatua kali za kisheria zinachukuliwa haraka dhidi ya watuhumiwa
kwa kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria,”