Ahukumiwa Miaka 92 Kisa Bangi Mtwara

Ahukumiwa Miaka 92 Kisa Bangi Mtwara

Mahakama ya Wilaya ya Nanyumbu imemuhukumu kifungo cha miaka 92 jela Salumu Yohana Mkonya (54) Mkulima na Mkazi wa Kiji cha Mnazimmoja, kwa makosa ya kupatikana na mbegu na majani yamimea ya dawa za kulevya aina ya bangi, misokoto ya dawa za kulevya aina ya bangi pamoja na kupatikana na pombe haramu ya moshi.

Akitoa taarifa ya kesi ambazo Polisi imepata mafanikio Mahakamani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman amesema Mtuhumiwa huyo alikuwa akihifadhi dawa za kulevya pamoja na pombe haramu ya moshi katika nyumba yake kwa lengo la kujipatia kipato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button