Waliojirekodi Wapenzi Wajinsia Moja Wakamatwa
Waliojirekodi Wapenzi Wajinsia Moja Wakamatwa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linawashikilia Watuhumiwa wawili ambao ni Dickson Paul Tamba (27) Mjasiriamali, Mkazi wa Mkuti chini machinjioni Wilaya ya Masasi na Mohamed Ally Kajao (34) Mwalimu Shule ya Msingi Nanyani, Mkazi wa magomeni Wilaya ya Mtwara kwa kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Akitoa taarifa leo February 12,2025 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara SACP Issa Suleiman amesema tukio hilo lilifanyika mwezi January 2025 katika nyumba ya kulala Wageni (jina limehifadhiwa).
Taarifa ya Polisi imesema walikamatwa baada ya Dicks Paul Tamba kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile na Mwalimu Mohamed Kajao huku wakijirekodi video kisha kuisambaza video hiyo kwenye mitandao ya kijami.