Basigye Apelekwa Hospitali Akigoma Kula Gerezani.

Basigye Apelekwa Hospitali Akigoma Kula Gerezani

Mwanasiasa wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, aliyegoma kula wiki iliyopita, amekimbizwa hospitali baada ya afya yake kuzorota, amesema mbunge na mtangazaji wa televisheni nchini humo.

Mpinzani huyo wa muda mrefu wa isiasa na mkosoaji wa Rais Yoweri Museveni, amekuwa kizuizini katika kituo cha ulinzi wa hali ya juu katika mji mkuu wa Kampala tangu Novemba 2024.

Mawakili wake wamesema “alitekwa nyara’ katika nchi jirani ya Kenya alikosafiri na kusafirishwa kwa nguvu hadi Uganda, ambako alishtakiwa katika Mahakama Kuu ya Kijeshi (GCM) kwa makosa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kumiliki silaha kinyume cha sheria.

“Huku kukiwa na ulinzi mkali, Dk Besigye ameletwa kwenye kliniki katika Mall ya Kiji cha Bugolobi,” ameandika Francis Mwijukye, mbunge anayeshirikiana Besigye, kwenye chapisho kwenye mtandao wa X Jumapili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button