Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kubariki adhabu ya Mbunge wa kisesa Luhaga Mpina kutohudhuria vikao 15 mfululizo vya Bunge

Siku moja baada ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kubariki adhabu ya Mbunge wa kisesa Luhaga Mpina kutohudhuria vikao 15 mfululizo vya Bunge hivi ndio vikao ambavyo Mbunge huyo atavikosa wakati akitumikia adhabu yake.

👉🏼 Vikao Vitano vya Bunge la bajeti Mkutano wa 15 unaoendelea yaan kuanzia jana alipotolewa bungeni adhabu yake ilianza rasmi muda huo huo.

👉🏼 Vikao Tisa vya Bunge lijalo la mwezi August katika mkutano wa 16.

👉🏼 Kikao kimoja cha Bunge la Mwezi November 2024 na ataejea katika kikao cha pili cha Mkutano huo wa 17

Pamoja na kutekeleza adhabu hiyo Mbunge huyo hataruhusiwa kuonekana kwenye viwanja vya Bunge wala hataruhusiwa kufanya shughuli yoyote ya Kibunge wakati wa utekelezaji wa adhabu hii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button