FAHAMU KUHUSU KORONGO DOMO NGAZI (Africa’s Saddle-billed stork).

 

 

KWANINI AITWE DOMO NGAZI?
Kuna wakati majina hutolewa kulingana na maumbile, sauti, rangi, na mengineyo kama hayo. Sasa huyu korongo domo ngazi, imetokana na mdomo wake ulivyo na pingili pingili za rangi nyeusi na nyekundu. Angalia midomo yao.

WANA MIGUU MIREFU SANA.
Miguu hiyo mirefu ni faida kwake hasa kwenye mambo mawili makubwa:-

1. KUTAFUTA CHAKULA.
Inamsaidia anapokuwa akijitafutia chakula kwenye maji iwe ni bwawa, dimbwi, au popote pale. Huweza kutembea hata sehemu yenye kina kirefu kidogo.

2. KUONA MAADUI TOKA MBALI.
Humrahisishia kuona mbali kidogo, hivyo inakuwa rahisi kwake kuwaona maadui zake pale wanapomkaribia na kuchukua tahadhari.

NI NDEGE MREFU KIASI KWA KIMO.
Miguu yake inafikia sentimeta thelathini na sita na nusu (36.5cm), yeye mwenyewe anafikia mpaka urefu wa karibia sentimeta mia moja na hamsini (150cm).

ANAYEPENDA KUKAA PEKE YAKE MUDA MWINGI.
Hupendelea kukaa peke yake zaidi na huwa wawili wawili hasa wakati wa kuzaliana. Korongo domo ngazi anatajwa kuwa ni ndege mwenye aibu pia.

UNAWEZA KUJUA JINSIA KWA KUWAANGALIA MACHO YAO TU.
Kwa kawaida korongo domo ngazi jike huwa ni mdogo kuliko dume. Lakini unaweza kutazama macho yao na ukajua huyu ni dume au jike.

Jike huwa na macho yenye rangi ya njano (yellow eyes), wakati dume huwa na rangi ya dark brown, na ukimuangalia chini ya kichwa, utaona kuna vidude vya njano vinaning’inia, kitaalamu wanaviita wattles.

NI NDEGE JAMII YA WALA NYAMA.
Hula zaidi samaki, wadudu wa majini, vyura, ndege wadogo na hata mayai pia. Kutokana na kula nyama zaidi, mara nyingi utawakuta maeneo ambayo kuna maji karibu.

HAWANA SAUTI.
Moja kati ya jamii ya ndege ambao hawana sauti kutokana na kukosekana kwa baadhi ya organ ambazo zinazalisha mawimbi ya sauti kama ilivyo kwa baadhi ya ndege.

Hawa wanakosa kitu ambacho kitaalamu wanakiita SYRINX. Hiki ndo kinahusika na mfumo wa sauti kwa ndege wengine ambao unasikia wakitoa sauti na kuimba.

WANAISHI KWA MUDA MREFU KIDOGO.
Hawa nao wanafikia mpaka miaka 12 wakiwa porini na miaka 19 wakiwa wanafugwa,,ila rekodi kubwa inasema wanaweza kufikia mpaka miaka 30.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button