MFAHAMU MYAMA FISI ALIVYO SEHEMU YA PILI (FACTS ABOUT HYENA PART2)
SEHEMU YA 2.
Inaendelea toka post iliyopita nyuma (Continuation)
Nilisema fisi ni jamii ya wanyama ambao wanapata shida kubwa kwenye suala la uzazi, kitu ambacho hupelekea kupoteza watoto wengi ama fisi jike mwenyewe kufa kutokana na kukwaruzwa kwa njia yake ya uzazi hivyo kumletea majeraha na maumivu makubwa. 😪
NINI HUPELEKEA TATIZO HILI?
Tatizo la uzazi wa fisi hutokana na mambo kadhaa kama ifuatavyo:-
1. WINGI WA HOMONI MWILINI
Fisi jike ana wingi wa homoni ijulikanayo kama testosterone ambayo ni mara tatu zaidi kuliko ile waliyonayo fisi dume.
Kumbuka hii homoni ndo inayosababisha sehemu za jike za uzazi kukua zaidi hadi kufanana na za dume. Wingi wa homoni hii inatajwa kuchangia zaidi kuleta uchungu wakati wa kuzaa.
2. MAUMBILE YA UZAZI
Maumbile ya fisi jike ya uzazi yanafanana na ya dume (pseudo-penis) na kumbuka maumbile hayo ndo anayotumia kwa kuzalia, kukojoa na hata kujamiiana (Angalia picha ya 2 kwenye post hii utaona hayo maumbile ya jike yanavyoonekana). Huyo ni fisi jike na sio dume.
3. WEMBABA WA MAUMBILE YA UZAZI
Wembamba wa njia ya kuzalia kwa fisi jike ni nyembamba (kama nchi moja/sentimeta mbili na nusu) ukilinganisha na uzito wa watoto wanaozaliwa ambao ni wastani wa kilo moja na nusu.
Hii husababisha watoto wengi kukosa hewa na kushindwa kupumua vizuri (suffocation) na kupelekea kufa wakati wakiwa wanazaliwa.
WAKATI WA KUJAMIIANA, FISI JIKE NDO HUAMUA.
Kutokana na maumbile ya uzazi ya fisi jike kufanana na ya fisi dume. Husababisha changamoto sana kwenye kujamiiana, hivyo ili hili suala litimie, ni lazima fisi jike aamue na yeye ndo huchagua dume wa kumpanda. Kama dume atashindwa kazi, lazima apigwe. 😁👌
FISI WANA UWEZO WA KUHESABU.
Jamii ya fisi hasa fisi madoa inasemekana wana uwezo wa kuhesabu. Kama fisi ataamua kujiunga na ukoo mwingine, atafanya sensa ya haraka kujua ni ukoo gani mzuri wa yeye kujiunga.
Kwa mfano: Kama fisi dume ataamua kujiunga na ukoo mwingine, basi atatafuta ukoo wenye madume wachache, na kwa jike atatafuta ukoo wenye majike wachache ndo atajiunga nao.

Makala hii imedhaminiwa na winn licious