Jeshi La Polisi Latoa Tamko Jipya.

Jeshi La Polisi Latoa Tamko Jipya.

Jeshi la Polisi nchini limesema linaendelea kulinda usalama wa raia na mali zao, ili kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, huku likionya kama kuna ambaye atajitokeza na kukaidi kutii sheria za nchi kwa lengo la kuhatarisha usalama wa nchi na kusimamisha shughuli za kiuchumi na kijamii zisiendelee kama wanavyo hamasishana na kudanganyana, watawadhibiti ili nchi ibaki salama na Watanzania wema na wapenda amani wabaki salama.

Hayo yamebainishwa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, DCP David Misime, na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kufanya shughuli zao na kufuata maelekezo watakayo kuwa wanapewa na Vyombo vya Ulinzi na Usalama maeneo yote nchini na kutii sheria za nchi kwani hayo yote yanafanyika ili Taifa liendelee kuwa salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button