Kamati Ya Bunge Yaingilia Kati Matengenezo Ya MV Magogoni.

Kamati ya Bunge Yaingilia Kati Matengenezo Ya MV Magogoni.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imeielekeza Serikali kutoa fedha zilizoidhinishwa na bunge katika bajeti ya mwaka uliopita, ilikukamilisha malipo ya matengenezo ya kivuko cha MV Magogoni kilichopo nchini Kenya.

Kivuko hicho, kilipelekwa kwenye matengenezo makubwanMombasa nchini Kenya, Februari 2023 na iliahidi kingekamilika Agosti mwaka huo, lakini ni mwaka wa pili sasa bado hakijakamilika.

Hata hivyo, katika ripoti yake maalumu baada yanuchunguzi wa miezi mitatu, gazeti hili liliwahi kuripoti, licha ya kivuko hicho kupelekwa kwenye matengenezo Serikali ililipa asilimia 1 0 pekee ya Sh7.5 bilioni ilizopaswa kumlipa mkandarasi, African Marine and General Engineering Company Ltd, Agizo hilo, limetolewa leo Jumatatu Machi 17, 2025

Na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Suleiman Kakoso, alipokua katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya miundombinu, yakiwemo maegesho ya kivuko cha magogoni, Kigamboni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button