Kanye West amesema, ni heri angepata watoto na #ParisHilton kuliko Kim Kardashian.

Kanye West amesema, ni heri angepata watoto na #ParisHilton kuliko Kim Kardashian. Mawazo ya Kanye West ni kwamba, angepata watoto na Paris Hilton, basi angekuwa na hoteli nyingi sana zenye chapa ya Hilton.

Kanye ameuwaza utajiri wa familia ya Hilton ambao unafikia ($14.2 billion) ambapo pia wanamiliki hoteli zenye chapa hiyo ambazo zinafikia zaidi ya 500 kwenye mataifa 80 duniani kote.

Paris Hilton na Kim Kardashian walikuwa marafiki wakubwa tangu utotoni, lakini ushkaji wao uliingia dosari mwaka 2007 baada ya Kim kupata umaarufu. Kim alikuwa msaidizi wa Paris Hilton pia akimsaidia kwenye masuala ya urembo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button