Kanye west Aupa Mlima Kilimanjaro Kipaombele Kwenye Malengo Yake.
Kanye west Aupa Mlima Kilimanjaro Kipaombele Kwenye Malengo Yake
Rapa anayejulikana kwa kufikiria tofauti, Kanye West, amejikuta tena katikati ya gumzo la mitandaoni. Safari hii sio kwa muziki au fasheni, bali kwa #bucketlist inayodaiwa kuwa yake. Kilichowashangaza wengi ni kwamba namba 1 kwenye orodha hiyo ni kupanda Mlima Kilimanjaro.
Ndiyo, kabla ya ndoto za nyumba za kifahari, safari za duniani au miradi mingine mikubwa, Ye anaweka macho yake kwenye #MountKilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika. Kwa mtu aliyezoea kuwa juu ya chati na majukwaa, safari hii haina beat, haina macho ya mashabiki ni pumzi, baridi na kupambana na wewe mwenyewe.
Kupanda Kilimanjaro ni changamoto ya kimwili na kiakili, kitu kinachomtoa mtu kwenye kelele za mitandao na kumrudisha kwenye ukimya wa maumbile. Na kwa Kanye, hilo linafanana kabisa na falsafa yake ya “kujivunja ili kujijenga upya.”
Kwa Watanzania, hii ni sababu ya kutabasamu. Mlima wetu unazidi kuwa kivutio cha ndoto ya watu wakubwa duniani.
Wewe ungeanza na namba 1 ipi kwenye bucket list yako?






