Kisa Uhaba wa #Dola, Bei ya #Petrol, Dizeli ya Panda.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei mpya ya mafuta ya petroli hapa nchini itakayoanza kutumika Leo Siku ya Jumatano August 02, 2023 ambapo kwa mwezi August 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.
Kupanda kwa bei ya mafuta kwa mwezi Agosti 2023 ni kutokana changamoto ya upatikanaji wa Dola za Marekani, mabadiliko ya sera za kikodi, kushuka kwa thamani ya Shilingi dhidi ya Dola ya Marekani, ongezeko la gharama za mafuta katika soko la dunia na gharama za uagizaji wa mafuta.