Mapacha Wa Miaka 17 Simiyu Wafariki Wakitaka Kuongezewa Matiti Ili waolewe.

Mapacha wa Miaka 17, Wakazi wa Kijji cha Bubale Wilayani Bariadi wamepoteza maisha baada ya kudaiwa kuogeshwa dawa na Mganga wa Tiba Asili kwa lengo la kuwaongezea ukubwa wa Matiti ili waweze kuolewa.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Byuna, Dkt. Deogratius Mtaki amesema alianza kupokea Mwili wa Pacha wa Pili (Doto) na baadaye akampokea Pacha wa Kwanza (Kulwa) akiwa mahututi ambaye alipoteza maisha muda mfupi baadaye.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya #Bariadi, Simon Simalenga ametoa wito kwa Jeshi la Polisi Wilayani humo kuwachukulia hatua wote waliohusika na tukio hilo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button