Mwanahabari Aliyepinga Vita Vya Ukraine Ahukumiwa Miaka 8.5 Jela.

Mwandishi wa habari aliyeandamana ahukumiwa miaka 8.5 jela. Marina Ovsyannikova ambaye alishiriki maandamano wakati wa Matangazo Mubashara Live’ kwenye Runinga akipinga uvamizi wa Urusi dhidi ya  Ukraine amepewa hukumu hiyo bila yeye kuwepo Mahakamani.

Mahakama imeeleza Mwandishi huyo amekutwa na hatia ya “Kusambaza hadharani habari za uongo licha ya kuwa na ufahamu kuhusu matumizi ya
Vikosi vya Wanajeshi wa Urusi”.

Ovsyannikova anayeishi uhamishoni Paris, Ufaransa amesema “Ni hukumu isiyo na Haki, Urusi hakuna haki Mahakamani, Rais ameharibu mfumo, hata ushahidi waliotoa juu yangu ni wa uongo, ndugu zangu wa Urusi wanahisi wamezungukwa na maadui muda wote na nikirudi inamaanisha nitafikia jela.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button