Marekani Yaongeza Uzalishaji wa Bomu La Nyukilia B61-13.

Marekani Yaongeza Uzalishaji wa Bomu La Nyukilia B61-13.

Marekani imeanza kuzalisha kwa wingi bomu jipya la nyuklia la B61-13 kabla ya ratiba, kama sehemu ya juhudi zake za kisasa za kuboresha silaha za nyuklia.

Bomu hili lina uwezo wa miondoko ya mlipuko kutoka kilotani 10 hadi 360, likiboresha toleo la zamani la B61-7 kwa usalama, usahihi, na teknolojia ya kisasa B61-13 limeundwa kuchukua nafasi ya mabomu ya zamani bila kuongeza idadi ya silaha za nyuklia katika hifadhi.

Litabebwa na ndege za kivita za B-2 Spirit na B-21 Raider. Hatua hii ni jibu kwa vitisho vinavyozidi kuongezeka kutoka kwa mataifa hatarishi na upanuzi wa hazina ya silaha za nyuklia ya China,

Hatua hii inaonyesha kujitolea kwa Marekani katika kulinda usalama wa taifa na washirika wake, huku ikihakikisha uwezo wa kujibu mashambulizi ya kisasa kwa ufanisi zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button