Mtoto wa Museveni Adai Wanajeshi Wa Uganda Wataingia DRC Wakati Wowote.

Mtoto wa Museveni Adai Wanajeshi Wa Uganda Wataingia DRC Wakati Wowote.

Mkuu wa Majeshi nchini Uganda Muhoozi Kainerugaba, amesema askari wa Jeshi la
Uganda (UPDF) ama wapiganaji wa Kundi la M23 watawasili katika mji wa Kisangani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) chini ya wiki moja ijayo.

Katika chapisho lake la jana Jumapili Machi 23, 2025, Kainerugaba amesema wanajeshi wake ama M23 watawasili Kisangani kwa agizo la Rais Yoweri Museveni ambaye ni baba yake, ili kuwaokoa wakaazi wa Kisangani dhidi ya matendo yanayofanywa na makundi mengine ya waasi nchini DRC.

“Watu wetu wa Kisangani, tunakuja kuwaokoa. Jeshi la Mungu linakuja!” Kainerugaba aliandika kwenye X.


Aliongeza: “Ndani ya wiki moja, aidha M23 au UPDF (Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda) litakuwa Kisangani. Kwa amri ya Yoweri Museveni, Amiri Jeshi Mkuu wa UPDF!”

Kuchukuliwa kwa Kisangani na M23 kungesababisha kuongezeka kwa mgogoro, kwani kunaweza kuliingiza kundi hilo ndani zaidi ya ardhi ya DRC

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button