Mtoto wa rapa maarufu Lil Wayne, anayefahamika kama Lil Novi (jina halisi Neal Carter)baba yake nimkali zaidi kati ya Lil Wayne na Drake,
Mtoto wa rapa maarufu Lil Wayne, anayefahamika kama Lil Novi (jina halisi Neal Carter), amezua mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufunguka kuhusu uwezo wa Drake dhidi ya baba yake. Akiulizwa ni nani mkali zaidi kati ya Lil Wayne na Drake, Lil Novi alijibu kwa kujiamini kuwa baba yake ni mkali zaidi kwa sababu ameandika ngoma nyingi sana za Drake, na huenda bila msaada wake, leo hii Drake asingekuwa mahali alipo.
Kauli hiyo imezua gumzo na mijadala mingi, huku baadhi ya mashabiki wakipongeza ujasiri wake kuonyesha heshima kwa baba yake, lakini wengine wakimtuhumu kwa kiburi na kujaribu kupunguza mchango wa Drake katika muziki.
Ikumbukwe kuwa mwaka 2009, kupitia label ya Young Money Entertainment inayoongozwa na Lil Wayne, Drake alisainiwa rasmi na hapo ndipo safari yake ya mafanikio ilipoanza kwa kasi. Lil Wayne si tu alimsaini, bali pia alimsaidia katika utunzi, sauti, na kumfungulia milango ya kimataifa.
Hata hivyo, licha ya mchango huo mkubwa, kauli ya Lil Novi imepingwa vikali na baadhi ya mashabiki waliodai kuwa kama kweli Lil Wayne aliweza kumuandikia Drake ngoma kali, kwa nini basi hakufanya hivyo kwa albamu yake mpya “Tha Carter VI”?
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakiponda album hiyo wakidai haina ubunifu wa hali ya juu wala mvuto kama kazi zake za awali, jambo lililopelekea kuzuka kwa hoja kuwa huenda nyota ya Lil Wayne inaanza kufifia.
Pamoja na hayo, hakuna ubishi kuwa mchango wa Lil Wayne kwa wasanii kama Drake, Nicki Minaj, na wengine waliopitia Young Money ni mkubwa mno, lakini je, hiyo inamaanisha bila yeye Drake asingeweza kufika alipo leo? Dondosha Maoni yako.







