Fat Joe Ashtakiwa Kwa Unyanyasaji wa Kijinsia.

Fat Joe Ashtakiwa Kwa Unyanyasaji wa Kijinsia.

Rapa p kutoka Marekani, Joseph “Fat Joe” Cartagena, anakabiliwa na tuhuma nzito katika kesi mpya iliyofunguliwa na aliyekuwa mfanyakazi wake wa karibu, Terrance “T.A.” Dixon. Kesi hiyo yenye kurasa 157 iliwasilishwa tarehe 19 Juni kwenye Mahakama ya Wilaya ya Kusini mwa New York na wakili Tyrone Blackburn.

Dixon, ambaye alifanya kazi na Fat Joe kwa zaidi ya miaka 15 kama hypeman, mwandishi wa mistari, msanii wa sauti za nyuma (back vocal) na mlinzi, anadai alinyanyaswa kimwili, kisaikolojia, na kifedha kwa muda wote huo.

Anadai pia kuwa alishiriki kuandika na kuimba kwenye nyimbo kadhaa kama Congratulations na Ice Cream, bila kupewa stahiki wala kutambuliwa rasmi.

Kesi hiyo inamtuhumu Fat Joe kwa kuhusika na biashara ya ngono, hasa dhidi ya wasichana wadogo wa umri kati ya miaka 15 na 16, ambao walidaiwa kupewa zawadi, fedha, na hata upasuaji wa urembo. Mbali na hilo, Dixon anadai alilazimishwa kushiriki tendo la ndoa mara zaidi ya 4,000 akiwa chini ya vitisho mbalimbali vya kimwili na kisaikolojia.

Kwa upande wake, Fat Joe kupitia wakili wake Joe Tacopina, amekanusha vikali tuhuma hizo na kuzitaja kuwa za kutungwa kwa nia ya kulipiza kisasi baada ya msanii huyo kumfungulia Dixon kesi ya kashfa mwezi Aprili.

Kesi hiyo imechukua sura nzito na inatarajiwa kuendelea kusikika mahakamani huku pande zote zikiendelea kusimama kwenye misimamo yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button