Mwana Fa asisitiza kuendeleza kuunga mkono Michezo ya Aina Zote

Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma amesema Serikali itaendelea kuunga mkono michezo ya aina zote kuanzia ngazi ya chini ili kuwatia moyo wanamichezo wanaoanza na wale walioko kwenye tasnia hiyo hapa nchini.

Mhe. Mwinjuma ameyasema hayo usiku wa kuamkia Januari 2, 2024 baada ya kushuhudia mapambano ya ngumi yanayojulikana kama “Usiku wa Mawe Hananasif” yaliyofanyika Kinondoni, Dar es salaam.

Aidha, ametoa Rai kwa wawekezaji kutoka sekta binafsi wajitokeze kwa wingi kuwekeza katika mchezo wa ngumi ili kuwapa nafasi mabondia kuonekana.

“Sisi tumeelekezwa na Mhe. Rais kushuka chini kabisa kuhakikisha tunasimamia michezo yote, kuhakikisha kwamba tunavumbua, tunavilea na kuvitunza vipaji vingi kwenye michezo inayofanyika hapa nchini” amesisitiza Mhe. Mwinjuma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button