Nyuma ya mafanikio ya wachezaji wengi wa Kitanzania kuna Kijana anafanya kazi kubwa huyu ni Carlos_mastermind
Nyuma ya mafanikio ya wachezaji wengi wa Kitanzania kuna Kijana anafanya kazi kubwa huyu ni @carlos_mastermind Mmiliki wa Makampuni ya #Carlprolnternational #ProcentricInvestments
#CarlproFootbalISA .
Ndg @carlos_mastermind amekua bora katika kufanya scouting kwa Wachezaji wa ndani na nje huku akiwa vizuri kwenye branding haswa kwa nyota anaowasimania.
Carlos Sylvester anawasimamia ma nahodha wa Simba (Mohammed Hussein) na Yanga (Bakari Mwamnyeto) nje na nyota hao kuna Zawadi Mauya,Khomeiny Khomeiny,Kibu Denis,Mzamiru Yassin na Hussein Kazi.
Wachezaji waliochini yake wana mafanikio mengi ndani na nje ya uwanja,mfano halisi Tshabalala akiwa anatengeneza mpunga wa maana nje ya uwanja na wengineo wengi.
Amekua akifanya kazi pia na nyota wengi wa kigeni na moja ya timu amekua akifanya nao kazi ni Yanga SC na Simba SC.
NB.Picha hii @carlos_mastermind akiwa jukwaani na Nahodha wa Mamelodi Sundowns akiangalia mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliomalizika kwa suluhu mbele ya wenyeji Yanga SC.
Themba Zwane alikosekana jana uwanjani kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.