Polisi, RC, Chadema Wajadili Madai Yakutekwa Katibu wa Bavicha.
Polisi, RC, Chadema Wajadili Madai Yakutekwa Katibu wa Bavicha.
Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza imekanusha tuhuma za kuhusika katika kutoweka kwa Katibu wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) Mkoa wa Mwanza, Amani Manengelo ambaye inadaiwa alichukuliwa na watu waliojitambulisha ni maofisa wa polisi.
Manengelo anadaiwa kutoweka Februari 14, 2025, akiwa nyumbani kwa rafiki yake wa kike, Pendo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Wilbrod Mutafungwa amesema watu watatu, akiwemo Pendo, wanashikiliwa kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.
Akizungumza na viongozi wa Chadema waliojitokeza leo Jumatano Februari 19, 2025, katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kufuatilia hatima ya Manengelo, Mkuu wa mkoa huo, Said Mtanda, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, amesema Jeshi la Polisi halihusiki na kutoweka kwake.
“Tumefanya uchunguzi na hakuna taarifa zinazoonyesha kuwa Manengelo anashikiliwa katika kituo chochote cha polisi hapa Mwanza.
Aidha, waliomchukua kutoka kwa mtu anayefahamika kwa jina la Pendo si maofisa wa polisi,” amesema Mtanda.