Rais Kagame Amteua Binti Yake Wadhifa Nyeti.

Rais wa Rwanda Paul Kagame amemteua binti yake kushika wadhifa muhimu katika ofisi yake.

Bi Ange Kagame, 29, ameteuliwa kuwa naibu mkurugenzi mtendaji anayesimamia baraza la mikakati na sera, kwa mujibu wa taarifa za
kikao cha baraza la mawaziri kilichoongozwa na Rais Kagame siku ya Jumanne.

Bi Ange Kagame amekuwa akifanya kazi katika ofisi ya rais kama mchambuzi mkuu wa sera tangu 2019 akiwa na shahada za sayansi
ya siasa na masuala ya kimataifa kutoka vyuo vikuu vya Marekani.

Watoto wengine wawili wa Kagame pia wana nyadhifa serikalini. Mwanawe mkubwa, Ivan Kagame, aliteuliwa mwaka 2020 kwenye
bodi ya maendeleo ya Rwanda – ambayo ina jukumu la kuharakisha ukuaji wa uchumi kupitia sekta ya kibinafsi.

Mtoto wa tatu wa kiume, lan, ni afisa wa jeshi la ulinzi la Rwanda, na mwaka jana aliingizwa katika katika kikosi cha ulinzi wa rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button