Raisi Dkt. Hussein Mwinyi amepongeza kuanzishwa kwa programu ya “Jenga Kesho Iliyobora (BBT)
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi amepongeza kuanzishwa kwa programu ya “Jenga Kesho Iliyobora (BBT) – Mifugo na Uvuvi” na kubainisha kuwa programu hiyo ni moja ya suluhu za kutatua changamoto nchini.
Dkt. Mwinyi ameyasema hayo wakati wa mazungumzo na wadau kwenye mkutano wa kuonesha fursa za uwekezaji kwenye programu ya hiyo ya kielelezo.
Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam leo Septemba 7, 2023.
Pia Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa mkutano huo umelenga kuonesha fursa kwa wadau na kuwahamasisha kuunga mkono programu hiyo ya BBT.
Mkutano huo ni sehemu ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF) unaoendelea jijini
Dar es Salaam.