Serengeti Mbuga Namba Moja Tena Afrika.
Kwa mara nyingine tena Hifadhi ya Taifa Serengeti imeibuka Mshindi wa Tuzo ya Hifadhi bora Afrika kwa mwaka 2023(Africa’s Leading National Park 2023) ikiwa ni mara ya tano mfululizo.
Serengeti inaibuka kidedea kwa kushinda tuzo hii baada ya kuwazidi Washindani ambaoni Central Kalahari Game Reserve ya Botswana,
Etosha National Park ya Namibia, Kidepo Valley National Park ya Uganda, Kruger National Park ya South Africa, pamoja na Masai Mara National
Reserve ya Kenya.
Tuzo hiyo imetolewa na World Travel Awards’ usiku wa October 15, 2023 katika Falme za Kiarabu na kupokelewa na Mkuu wa Kanda ya Magharibi
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Izumbe Msindai kwa niaba ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).
Ushindi huu unaifanya Serengeti kuwa Hifadhi bora zaidi Afrika kwa miaka mitano mfululizo yaani mwaka 2019,2020,2021,2022 na 2023.
Tuzo za World Travel zilianzishwa mwaka 1993 ili kutambua, kutunza na kusherehekea ubora katika sekta zote muhimu ikiwemno sekta za usafiri, utalii na ukarimu, leo hi World Travel Awards inatambulika Duniani kote kama alama mahususi ya ubora wa tasnia mbalimbali.