SPIKA DKT. TULIA ACKSON AFUNGUA KONGAMANO LA WASOMI WA AFRIKA UDSM

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 29 Aprili 2025, amefungua rasmi Kongamano la Wasomi na Wanazuoni wa Afrika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Akizungumza wakati wa ufunguzi, Mhe. Spika amesisitiza umuhimu wa kulinda uhuru wa wanataaluma kama msingi wa maendeleo endelevu barani Afrika. Aidha, amewataka wanazuoni kutumia maarifa yao kuchochea mabadiliko chanya katika jamii.

Kongamano hilo limeandaliwa na Ndaki ya Sayansi za Jamii ya UDSM kwa kushirikiana na Kanseli ya Maendeleo ya Utafiti katika Sayansi za Jamii (CODESRIA) na linatarajiwa kudumu kwa siku nne, likijadili nafasi ya uhuru wa kitaaluma katika Afrika ya leo

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button