Tume: No reforms, no election, Samia must go na Oktoba Tunatiki zilichochea vurugu

Tume: No reforms, no election, Samia must go na Oktoba Tunatiki zilichochea vurugu

Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mohamed Chande, amesema baadhi ya kauli za No reforms, no election, Samia must go na Oktoba tunatiki ni baadhi ya vichocheo vya vurugu za Oktoba 29, 2025.

“Kauli za baadhi ya wanasiasa ambazo ziligeuka na kuwa kauli mbiu za baadhi ya waliokuwa wakifanya ghasia, No reforms, No election, Oktoba Tunatiki, Oktoba Tunatoka, Samia must go, wengine ni waliokatwa kwenye kugombea katika ngazi ya vyama, wakaona ghasia zilizokuwa zinafanywa zingewasaidia chini kwa chini,” amesema Jaji Chande.

Ameyasema hayo leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha akipokea Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Jaji Chande amesema baadhi ya kauli za No reforms, no election na Oktoba tunatiki ni baadhi ya vichocheo vya vurugu za Oktoba 29.

Oktoba 29, 2025 Tanzania ilikumbwa na vurugu kwenye maeneo mbalimbali nchini na kusababisha vifo, uharibifu wa miundombinu na mali za umma na watu binafsi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button