Tume: Hakuna uthibitisho wa uwepo wa makaburi ya halaiki
Tume: Hakuna uthibitisho wa uwepo wa makaburi ya halaiki
Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Othman Chande amesema uchunguzi uliofanyika umebaini hakuna uthibitisho wa uwepo wa makaburi ya halaiki kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa.
Akiwasilisha matokeo ya uchunguzi, Jaji Chande amesema uchunguzi wa kina umebaini madai hayo hayana ukweli.
Amesema tume ilitembelea na kukagua eneo la Makaburi ya Kondo, kufanya mahojiano na wasimamizi pamoja na kushirikisha wataalamu mbalimbali kufanya uchunguzi wa kisayansi, ikiwemo matumizi ya picha za satelaiti.
Amesema pamoja na hatua hizo, mazingira ya eneo hilo likiwa limezungukwa na makazi ya watu na kulindwa muda wote yalisaidia kufikia hitimisho kuwa hakuna ushahidi wa kuwepo makaburi ya halaiki.8
“Hivyo kwa kuzingatia hali halisi ilivyo pamoja na taarifa za uchunguzi wa kisayansi, tume ilibaini madai hayo hayakuweza kuthibitika,” amesema.



