Tume: Vijana waliwekwa kambini, kupewa mbinu kuvuruga uchaguzi

Tume: Vijana waliwekwa kambini, kupewa mbinu kuvuruga uchaguzi

Uchunguzi wa Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani umebaini kuwepo kwa dalili za kupanga na kuchochea ghasia za uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 zilianza kujitokeza miezi sita kabla ya siku ya kupiga kura hasa kupitia mitandao ya kijamii.

Akiwasilisha taarifa hiyo, leo Aprili 23, 2026 Mwenyekiti wa Tume, Jaji Othman Chande amesema kuwa kuanzia Aprili hadi Oktoba 2025, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilikuwa ikiwasilisha taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama zikionesha kuwepo kwa viashiria vya ghasia vinavyolenga kuzuia na kuvuruga uchaguzi.

Kwa mujibu wa Jaji Chande, Oktoba 17, 2025, TCRA iligundua kusambazwa kwa bango lenye maudhui ya kuchochea ghasia, likihamasisha maandamano yenye lengo la kuzuia na kuvunja uchaguzi mkuu.

Mbali na hilo, uchunguzi ulibaini mijadala mitandaoni iliyokuwa ikiendelea kuhusu mikakati ya kutekeleza ghasia siku ya uchaguzi.

“Majadiliano hayo yalionesha kuwa siku ya uchaguzi baadhi ya watu walipanga kuharibu mifumo ya umeme ili kuiingiza nchi gizani, kuchoma moto vituo vya mafuta pamoja na vituo vya kupigia kura kwa lengo la kuvuruga uchaguzi mkuu. Kwa mujibu wa uchunguzi huo, kulikuwa na vijana wasiopungua 500 waliokuwa wakihifadhiwa katika majengo, misitu na makambi mbalimbali nchini kwa takribani siku 28, wakipewa mafunzo maalumu kwa ajili ya kutekeleza ghasia siku ya uchaguzi,” amesema Jaji Chande.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button