Tume: Watu 518 walifariki ghasia za Oktoba 29
Tume: Watu 518 walifariki ghasia za Oktoba 29
Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imesema kuwa vifo vilivyotokana na ghasia hizo ni 518 ambao wanaume 490 sawa na asilimia 94.6, wanawake 28 sawa na asilimia 5.4, ambapo katika vifo hivyo watoto walikuwa 21.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji mstaafu, Mohamed Chande leo Alhamisi, Aprili 23, 2026 Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha akipokea Ripoti ya Tume hiyo kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan..
“Mkoa wa Dar es Salaam ulikuwa na vifo vingi zaidi ikiwa na vifo 182 ikiuatiwa na Mwanza 90, Mbeya 80 na Arusha 53,’ amesema Jaji Chande.




