Waziri wa Zamani wa Zambia Auwawa katika Operesheni Yakiusalama
Waziri wa Zamani wa Zambia Auwawa katika Operesheni Yakiusalama
Aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Zambia, Mutotwe Kafwaya, ameuawa wakati wa operesheni ya kiusalama katika eneo linalohusishwa na kiongozi wa upinzani, Brian Mundubile, polisi wamethibitisha. Kifo hicho kimeongeza sintofahamu na wasiwasi wa kisiasa nchini humo kufuatia uchaguzi wa urais wa Agosti 13,2026.
Polisi wamesema Kafwaya alijeruhiwa kwa risasi na kufariki wakati vikosi vya usalama vilipambana na watu wasiojulikana katika operesheni hiyo. Kwa siku kadhaa, taarifa kuhusu alikokuwa Kafwaya hazikuwa wazi. Familia yake na viongozi wa upinzani walitaka Serikali kutoa taarifa, huku taarifa za awali zikidai alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Kijeshi ya Maina Soko.
Hata hivyo, maofisa wa Serikali walikanusha taarifa hizo, wakisema hakuna mgonjwa mwenye jina hilo aliyekuwa hospitalini hapo. Polisi sasa wamesema vikosi vya usalama vilifyatuliwa risasi na kulazimika kujibu mashambulizi hayo. Mamlaka zilisema operesheni hiyo ililenga kuwakamata watu waliokuvwa wakishukiwa kujihusisha na shughuli za wanamgambo na waliokuwa tishio kwa usalama wa Serikali.





