Wafia Kwenye Helikopta Wakienda Honeymoon

Wafia Kwenye Helikopta Wakienda Honeymoon

Wanandoa Marie Ebert (30) na Alexander Cromie (31) wamefariki dunia baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka katika Kisiwa cha Sifnos Nchini Greece, walikokuwa wamekwenda kwa ajili ya fungate yao baada ya kufunga ndoa hivi karibuni.

Ajali hiyo pia imesababisha kifo cha rubani Giorgos Raikos (53), raia wa Greece na aliyekuwa Afisa wa Jeshi la Anga mwenye uzoefu mkubwa ambapo helikopta hiyo aina ya Bell 206 inadaiwa kutoa sauti isiyo ya kawaida kabla ya kuanza kuzunguka bila udhibiti na kuanguka takribani mita 50 kutoka eneo ililotakiwa kutua.

Baada ya kugonga ardhi, helikopta hiyo ililipuka na kushika moto, huku Waokoaji waliowasili eneo la tukio wakikuta Watu wote watatu waliokuwa ndani yake wamefariki. Mamlaka Nchini Greece zimeanza uchunguzi kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo, huku hitilafu ya kiufundi ikitajwa kuwa miongoni mwa mambo yanayochunguzwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button