Trump Aanzisha Vita vya Kiuchumi dhidi ya Iran Atoa Onyo

Trump Aanzisha Vita vya Kiuchumi dhidi ya Iran Atoa Onyo

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza hatua mpya za kuongeza shinikizo la kiuchumi dhidi ya Iran, akisema nchi na taasisi zitakazoendelea kuipa Tehran msaada wa kifedha, kibiashara au vifaa zitakabiliwa na madhara makubwa ya kiuchumi. Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa Truth Social, leo Agosti 20,2026, Trump amesema Marekani imeanzisha kile alichokita operesheni kubwa ya kiuchumi dhidi ya lran, akiahidi kuiongezea vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa.

Hatua hizo zinalenga pia biashara ya mafuta ya Iran pamoja na njia zinazotumiwa kukwepa vikwazo vya Marekani, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Washington kuishinikiza Tehran ikubali makubaliano mapya ya nyuklia yenye masharti makali zaidi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Reuters, kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Trump kusema hakuna mazungumzo yanayoendelea kati ya Marekani na Iran wala yaliyopangwa kwa sasa. Amesisitiza kuwa Iran ilipoteza nafasi ya kufikia makubaliano, huku akitaka ikubali masharti ya Marekani.

Iran imekataa msimamo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Abbas Araqchi, amesema Tehran iko tayari kwa mazungumzo, lakini haitakubali masharti yanayolazimisha kusalimu amri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button