Baba Safirini, Mke na Watoto Wakauawa
Baba Safirini Mke na Watoto Wakauawa
Fabiano Mkeza ambaye ni Baba wa familia ya Asha Lukonge na Hashim Fabiano ameibua simanzi wakati wa mazishi ya Mke na Mtoto wake, wanaodaiwa kuuawa kwa kunyongwa na Ndugu wa familia hiyo, Anderson Bosco.
Mazishi hayo yamefanyika leo Agosti 18, 2026 katika Makaburi ya Azimio, Kilosa Mjini baada ya tukio hilo kutokea Agosti 15, 2026 katika Kiji cha llakala, Kata ya Mhenda, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro.
Inadaiwa kuwa tukio hilo lilitokea wakati Fabiano akiwa safarini, ambapo Anderson ambaye awali alifika katika familia hiyo kwa lengo la kufanya vibarua, anadaiwa kumuua Asha pamoja na Mtoto wake kwa kuvwanyonga, kisha kuwafukia nyuma ya nyumba yao.
Baada ya tukio hilo, Mtuhumiwa huyo anadaiwa pia kuuza magunia nane ya mahindi yaliyokuwa yamehifadhiwa kwa ajili ya chakula kwa shilingi 300,000, ambapo Jeshi la Polisi limesema linaendelea na msako wa kumtafuta Bosco ambaye anadaiwa kukimbia baada ya tukio hilo na hadi sasa hajulikani alipo.





