Matonya Aitaka Kolabo ya Chino na Christian Bella.

Matonya Aitaka Kolabo ya Chino na Christian Bella

Msanii Chino Kidd amewagusa mashabiki
wake kwa kushare video akiwa na mama yake pamoja na watu wengine wakifurahia muziki. Katika video hiyo, wimbo wa Chino Kidd unaosikika utakuwa sehemu ya EP
yake ijayo.

Chino amemshirikisha msani nguli Christian
Bella kwenye wimbo huu wa kipekee, ambao utakuwa track ya nne kwenye EP hiyo.
Kupitia caption yake, Chino ameeleza upendo wake kwa mama yake na juhudi anazofanya kwa ajili ya familia yake,
akiandika:

“Love your mom.. unajua mwanao napambana sana kwa ajili yenu. Umenifunza kusali, subira na upendo kwa kila anaenizunguka.”

Alimwombea Mungu aendelee
kumtunza mama yake ili aendelee kufurahia matunda ya juhudi zake.

Msanii mkongwe, @matonyambili, alijumuika kwenye maoni, akimsihi @Christian Bella1 wafanye remix ya wimbo huo na @chino_kidd7, akisema, “Bella, tuweke
remix na kijana wetu sawa.” Hii inaongeza hamu kwa mashabiki ambao wanaisubiri EP hiyo kwa hamu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button