Aliyemuua Mkewe Kisha Kumchoma na Magunia Ya Mkaa Ahukumiwa Kunyongwa

Aliyemuua Mkewe Kisa Kumchoma na Magunia Ya Mkaa Ahukumiwa Kunyongwa

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemuhukumu kunyongwa hadi kufa mfanyabiashara Hamis Luwongo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mke wake, Naomi Marijani.

Hukumu hiyo imetolewa Leo Februari 26,2025 na Jaji wa mahakama hiyo, Hamidu Mwanga baada ya kuridhishwa na ushahidi uliyotolewa na upande wa mashtaka ambao ulikuwa na mashahidi 14 na vielelezo 10.

Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, jopo la mawakili wa serikali uliiomba Mahakama kutoa adhabu Kali dhidi ya mshtakivwa ili iwe fundisho kwa wanaume wanaofanya vitendo vya kikatili kwa wanawake zao kwa kigezo kuwa wapo katika ndoa.

Katika kesi ya msingi, Luwongo alikuwa anakabiliwa na shtaka la mauaji ya mkewe Naomi kinyume na kifungu cha sheria cha 196 na 197 cha sheria na Kanuni ya adhabu kama ilivyorejewa mwaka 2019.

Mshtakiwa Luwongo ambaye ni mkazi wa Kigamboni Dar es Salaam alidaivwa Mei 15,2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua mkewe Naomi Marijani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button