Diamond Kutoana Jasho na Burna Boy, Asake Tuzo Trace Muziki leo.
Diamond Kutoana Jasho na Burna Boy, Asake Tuzo za Trace Muziki Leo.
Moja ya tukio ambalo linasubiriwa kwa hamu Zanzibar kisiwani Unguja ni ugawaji wa Tuzo
za Trace ambazo zinatarajiwa kutolewa usiku wa leo Jumatano, Februari 26,2025.
Tukio hilo ambalo lilianza mapema jana linatarajiwa kuendelea kuwakaribisha mastaa kutoka mataifa mbalimbali.
Katika usiku huo jukwaa litatawaliwa na wasanii wazawa akiwemo Diamond Platnumz, Jux, Zuchu, Harmonize,
Alikiba, Marioo, Abigail Chams, Mbosso, Lunya, Bella Kombo na Nandy.
Mbali na hao wapo wasanii kutoka nje ya Tanzania kama Rema, TitoM & Yuppe, Joé Dwèt Filé, Fally Ipupa, Didi B, Tyler ICU, Qing Madi, Bien, Innoss’B, Yemi Alade, Black
Sherif na wengineo.
Hivyo basi tuzo hizo zitawakutanisha wasanii zaidi ya 300 wa kimataifa huku wakitoana jasho katika vipengele mbalimbali.
Ambapo Diamond anakuwa msanii pekee
kutoka Bongo anayewania tuzo katika kipengele cha ‘Song Of The Year kupitia ngoma ya ‘Komasava’.