Kumbukizi Ya Miaka Minne Ya Kifo Cha Magufuli

Kumbukizi Ya Miaka Minne Ya Kifo Cha Magufuli.

LEO Machi 17, ni kumbukizi ya miaka minne tangu Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Dk John Pombe Magufuli, afariki dunia.

Dk Magufuli alifariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena, mkoani Dar es Salaam na alizikwa Machi 26, 2021 nyumbani kwake Chato, mkoani Geita, Dk Magufuli alizaliwa Oktoba 29, 1959 huko Chato, na alitumikia nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia Novemba 5, 2015 hadi umauti ulipomfika.

Wakati akitangaza msiba huo kwa taifa, Makamu wa Rais wa wakati huo na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan alisema Dk Magufuli alifariki dunia kutokana na tatizo la mfumo wa umeme wa moyo (heart rhythm disorder).

Katika kipindi cha uongozi wake, Dk Magufuli alijulikana kwa msimamo thabiti katika kusimamia uwajibikaji serikalini, mapambano dhidi ya rushwa, na juhudi za kuanzisha miradi mikubwa ya maendeleo kama ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR), Bwawa la Nyerere, na upanuzi wa huduma za afya na elimu.

Unamkumbuka Mgafuli kwa lipi?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button