Mhe. Ummy Mwalimu leo Januari 18, 2023 amewasilisha Maazimio ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Januari 18, 2023 amewasilisha Maazimio ya Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Wizara ya Afya kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Dkt. Faustine Ndugulile.
Miongoni mwa hoja alizowasilisha ni pamoja na Uwekezaji wa viwanda vya dawa na vifaa tiba kufanywa na Bohari ya Dawa, Uingizwaji nchini wa bidhaa bandia za chakula, dawa na Vipodozi pamoja na Dawa za Asili.
Wazir @ummymwalimu ameambatana na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel, Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Grace Magembe, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu pamoja na Wakurugenzi kutoka Wizara ya Afya.








