Ronaldo Bado kumbe Sana
NYOTA wa Al-Nassr, Cristiano Ronaldo amesisitiza hafikirii kustaafu soka na ataendelea kucheza soka siku za usoni. Kauli ya Ronaldo 38, ilikuja baada ya kufunga mabao mawili kwenye ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Al-Ahli wikiendi iliyopita.
“Napenda sana soka licha ya umri wangu kwenda, napenda kufunga na kucheza, kushinda mechi na nitaendelea kufanya hivyo hadi miguu yangu iseme inatosha. “Najisikia vizuri sana, nitaisaidia timu yangu. Lakini jambo la msingi kabisa tupo kileleni mwa msimamo wa ligi kwa sasa,” alisema.
Ronaldo amefikisha mabao tisa pia, ametoa asisti sita katika mechi sita alizocheza mpaka sasa. Wachambuzi wa soka Saudi walishangazwa na ushindani wa Ronaldo licha ya kuwa ya kuwa na umri wa miaka 38 baada ya kujiunga na Al-Nassr