Cristiano Ronaldo Akosa Muda wakufikisha Magoli 1000

Cristiano Ronaldo Akosa Muda Wakufikisha Magoli 1000

Cristiano Ronaldo ameweka wazi kuwa
huenda asiweze kufikia lengo lake la mabao 1,000. Huku akiwa anakaribia umri wa miaka 40, mchezaji huyo wa Al Nassr na timu ya taifa ya Ureno amekiri kwamba hawezi
tena kupanga mipango ya muda mrefu kama zamani.

Ronaldo, aliyefikisha mabao 900 hivi karibuni, amesema, “Sasa naishi kwa wakati uliopo. Siwezi kufikiria mbali kama mwanzo. Nikifika mabao 1,000, itakuwa vyema, lakini hata nisipofika, tayari mimi ni mfungaji bora kwenye historia.”

Hivi majuzi, Ronaldo alitunukiwa tuzo ya juu kabisa nchini Ureno, Platinum Quinas, kwa mchango wake kwa timu ya taifa kwa zaidi ya miaka 20. Rais wa Shirikisho la Soka la
Ureno, Fernando Gomes, alimsifu Ronaldo kwa kujitolea na kuwa balozi bora kwa nchỉ yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button