Tyla Anunua Cheni ya Tsh Bilioni 2.6

Tyla Anunua Cheni ya Tsh Bilioni 2.6

Msanii Kutoka Nchini Afrika Kusini @tyla Amenunua Cheni Yenye Thamani Ya Dola Milioni 1 (Tsh BILIONI 2.6/=).

Hii Ni Baada Ya Kuonekana Akiwa Amevaa Cheni Hiyo Kwenye Usiku Wa Tuzo Za ‘MTV EMA Juzi Jumapili Huko Mjini Machester, Nchini Uingereza.

Kampuni Ya Vito Vya Thamani ‘Jacob & Cơ’ Imethibitisha Msanii Huyo Kununua Cheni Hiyo Kwa Kiasi Hicho Kikubwa Cha Fedha, Kwani Kupitia Ukurasa Wao Wa Instagram Wametumia Picha Ya Tyla Kumpongeza Kwa Ushindi Wake Wa Tuzo 3 Za Mtv Ema Huku Akiwa Amependeza Na Cheni Kutoka Kampuni Yao

.”Hongera Tyla Kwa Ushindi Wa Tuzo Za MTV EMA, Pamoja Na Kufurahia Mafanikio Huku Ukiwa Umevalia Cheni Ya Tsh Bilioni 2.6/=”

Tyla Ni Moja Kati Ya Wasanii Wenye Mafanikio Makubwa Ya Kimuziki Tangu 2023, Akionesha Uwezo Wake Kwa Kushinda Tuzo Kubwa Mbalimbali Kama; Grammy (1),Billboard (2), VMA (3), BET (4), MTV EMA

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button