Yafahamu Maswahibu Wanayopitia Walimu Shule Binafsi.

Yafahamu Maswahibu Wanayopitia Walimu Sekta Binafsi.

Unatambua kuwa walimu shule binafsi wanafanya kazi katika mazingira magumu
ikiwamo kukosa kinga na usalama wa ajira zao?

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu wa Shule Binafsi Tanzania (TPTU), Julius
Mabula, anayeelezea masaibu wanayopitia walimu wa shule hizo na masuala mengine mbalimbali kuhusu walimu na kada ya ya ualimu kwa jumla.

Akielezea masaibu hayo, Mabula amesema: “Changamoto ya kwanza ni ajira. Huku kwetu, ajira za walimu binafsi hazina kinga kama ilivyo kwa walimu wa Serikali, kwa
sababu ili umfukuze mwalimu ukutane na vyombo vitano, ambavyoni Wizara ya Elimu, Utumishi wa Umma, Tamisemi, CWT na Utumishi wa Walimu.

“Lakini huku sekta binafsi, mwajiri akikohoa kidogo umeshafukuzwa, kwa hiyo hiyo ndio inafanya watu kuona hiyo sio kazi, amesema na kuongeza Mabula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button