S2kizzy Azianika Hits Alizofanya Mwaka Huu

S2kizzy Azianika Hits Alizofanya Mwaka Huu.

S2Kizzy, mmoja wa watayarishaji
wakubwa wa muziki nchini Tanzania, ameendelea kung’aa mwaka 2024 kwa kutoa nyimbo nyingi zinazotamba
kupitia studio yake, @plutorepublic !..

Orodha hii ya nyimbo inayoanzia Januari hadi Septemba 2024 imejumuisha ngoma kali kama vile Komasava ya @DiamondPlatnumz na Ova ya @mbosso_ iliyotoka jana.

Mbali na Komasava, ambayo inamshirikisha Diamond Platnumz pamoja na Khalil Harrison na Chely, nyingine zilizomo kwenye orodha hiyo ni Hakuna Matata ya @marioo_tz, Ololufe Mi ya @Juma_Jux, na DAH! ya @officialnandy.

S2Kizzy ameendelea kuthibitisha uwezo wake wa kubadilisha muziki wa BongoFleva Kwa kuwafanya wasanii wa nyumbani kufanya muziki wa viwango vya Kimataifa.

Orodha inaonyesha ufanisi wake wa hali ya juu kwenye kuzalisha hits nyingi kutoka kwa wasanii maarufu kama @officialzuchu, @harmonize_tz, Nandy, na @billnass,
@officialalikiba, @countrywizzy_tz, @abigail chams na wengine, huku akitoa midundo yenye ushawishi ndani ya kipindi cha miezi tisa tu ya mwaka 2024.

Hit Gani Unaikubali Kutoka Kwa S2Kizzy Mwaka Huu?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button