Serikali ya Tanzania imehakikisha soko jipya nchini China linapatikana kwa mazao ya Alizeti, Tumbaku, Pilipili na Parachichi kufuatia kusainiwa Hati ya Makubaliano kati ya nchi hizo mbili tarehe 14 Agosti 2024.

Hati hiyo imesainiwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) na Waziri wa Mamlaka ya Forodha ya Watu wa China, Mhe. Yu Jianhua.
Makubaliano haya yatapanua soko la Alizeti, ambapo mashudu ya Alizeti yataweza kusafirishwa moja kwa moja kwenda China. Vilevile, makampuni tisa kutoka Tanzania sasa yataweza kusafirisha parachichi moja kwa moja nchini China