Uchumi wa Tanzania wapanda kwa 5.2%.
Uchumi wa Tanzania umeonyesha kukua kwa asilimia 5.2 katika robo ya pili ya mwaka 2023, ishara inayoonesha ahueni baada ya athari za janga la UVIKO-19 pamoja na vita vya Urusi na Ukraine.
Hii inathibitisha ukuaji chanya ikilinganishwa na miaka miwili iliyopita, ambapo ulikua kwa asilimia 4.7 mwaka 2022 na asilimia 3.8 mwaka 2021.
Sekta zilizorekodi ukuaji mkubwa zaidi ni huduma za kifedha na bima, ambazo zilikuwa na ukuaji wa asilimia 15.6, ikifuatiwa na sekta ya umeme (asilimia
12.4), na sekta myingine ikiwemo burudani (asilimia 11.5).
Sekta ambazo zinaajiri watu wengi, kama vile kilimo, ujenzi, biashara na ukarabati, zilirekodi ukuaji wa wastani.