Wanafunzi 121 wa UDOM Waondolewa Masomoni.

Wanafunzi 121 wa UDOM Waondolewa Masomoni.

Wanafunzi 121 wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), wameondolewa katika masomo (discontinue) kwa tuhuma za kuchezea matokeo, huku kesi 15 zikiendelea na uchunguzi zaidi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano na masoko cha chuo hicho, jumla ya.wanafunzi 170 walituhumiwa kuchezea mfumo matokeo (SR2) mwaka 2023/24.

“Serikali iliunda kikosi kazi kilichohusisha wataalamu wa mfumo wa kompyuta kuchunguza tuhuma hizo na kuwasilisha ripoti Chuo Kikuu cha Dodoma’imeeleza

  1. taarifa hiyo.Imebainisha baada ya kupokea ripoti hiyo hatua za ndani zilianza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwapa wito watuhumiwa kufika chuoni hapo kusikilizwa kabla ya kutoa uamuzi kwa mujibu wa kanuni.

“Jumla ya wanafunzi 148 walisikilizwa, wanafunzi 32 hawakufika kusikilizwa. Katika wanafunzi waliosikilizwa 121 walipatikana na hatia kuhusika na kuchezea matokeo ya mitihani na kikao cha seneti ya chuo kilipitisha kuondolewa masomoni.”

Taarifa hiyo imeeleza kuwa kesi za wanafunzi 15 zinaendelea na uchunguzi zaidi huku wanafunzi wakikutwa hawana hatia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button