Alicia Keys Ametimiza Miaka 15 ya ndoa na mumewe Swizz beat

Mtayarishaji maarufu wa muziki kutoka Marekani, Swizz Beatz, pamoja na mkewe, mwimbaji Alicia Keys, leo Julai 31, 2025 wametimiza miaka 15 ya ndoa tangu walipofunga pingu za maisha mnamo Julai 31, 2010.

Wanandoa hao wamebarikiwa kupata watoto wawili: Egypt (aliyezaliwa 2010) na Genesis (2014).

Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, Swizz Beatz na Alicia Keys wameonesha furaha yao kwa kufikia hatua hiyo ya ndoa, wakimshukuru Mungu kwa ulinzi na upendo aliowawezesha kwa miaka yote hiyo. Wameeleza pia dhamira yao ya kuendelea kupendana milele na kuendeleza familia yao kwa mshikamano na upendo thabiti.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button